Thursday, September 20, 2018

Kocha wa Juventus  Massimiliano Allegri anaamini kwamba Cristiano Ronaldo asingeoneshwa kadi nyekundu dhidi ya Valencia kama VAR ingekuwa inatumika mashindano ya UEFA.

Ronaldo alionekana kuweka mkono wake juu ya kichwa cha beki Jeison Murillo ambaye alikuwa chini dakika ya 29 , ambapo mwamuzi nyuma ya goli alitoa taarifa kwamba kuna kosa limefanywa na Ronaldo.

Mwamuzi wa Kijerumani Felix Brych aliwasiliana na mwamuzi mwenzake na kuamua kumtoa nje Ronaldo kwa kadi nyekundu.

Ronaldo akitokwa na machozi alitoka uwanjani lakini kocha wake Allegri amesisitiza kwamba , kadi nyekundu asingepata kama UEFA wangepitisha matumizi ya VAR kwenye haya mashindano.

"Ninachoweza kusema ni kwamba VAR ingeweza kumsaidia mwamuzi kufanya maamuzi sahihi . Zaidi ni kwasababu ilikuwa dakika ya 29 kipindi cha kwanza katika mechi ngumu , kujikuta na wachezaji 10 kwa kadi nyekundu , hiyo haikuwa sahihi."

0 comments:

Post a Comment