Kocha wa Bayern Munich Niko Kovac amekiri ni vigumu kwa Robert Lewandowski kuondoka Bayern Munich licha ya kuwepo kwa ripoti kuwa Real Madrid wameonesha nia ya kumuhitaji
Awali wakala wa Lewandowski Pini Zahavi alithibitisha kuwa mteja wake anamatumaini kuwa ataondoka Allianz Arena na kocha Kovac alikuwa anatambua hilo.
Swala hili la kuhusu kuhusishwa kwa Lewandowski na vilabu vingine liliongezewa chachu na Mtendaji mkuu wa Borussia Dortmund Hans-Joachim Watzke baada ya kuonesha nia ya kutaka kulipa Euro milioni 100 kuipata saini ya Lewandowski .
Lakini taarifa mpya hivi sasa zinaeleza kuwa Kovac,hayupo tayari kupoteza huduma ya mshambuliaji huyo. "Hakuna jambo jipya kuhusu Robert, ni wazi kuwa hataondoka klabuni kwa sababu nimshambuliaji wa daraja la juu na hivyo hatupendi kumuacha aende" alisema Kovac akiongea na Skysport German.
0 comments:
Post a Comment