Mesut Ozil ametangaza rasmi kujiuzulu kuitumikia timu ya taifa ya Ujerumani kupitia barua yake ya wazi aliyoisambaza kwenye mitandao ya kijamii.
Ozil ameeleza kwamba uamuzi wake huo unatokana na namna baadhi ya viongozi wa shirikisho la soka la Ujerumani (DFB) kutomuheshimu na kumbagua kutokana na asili yake ya nchi ya Uturuki.
Ozil amekuwa akisemwa sana na baadhi ya wanasiasa wa Ujerumani wakimuita msaliti baada ya kuonekana kwenye picha ya pamoja na kiongozi wa taifa la Uturuki - Rais Erdogan - na maneno dhidi yake yalizidi zaidi wakati Ujerumani ilipokuwa kwenye mashindano ya Kombe la dunia ambapo walitolewa kwenye makundi. Ozil amewatuhumu viongozi wa shirikisho kumgeuza yeye mbuzi wa kafara na kumtumia kwenye propaganda za kisiasa.
Sunday, July 22, 2018
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment