Saturday, January 6, 2018

  Siku chache zilizopita Jose Mourinho alisema kuwa baadhi ya makocha wa EPL wanakuwa waigizaji katika eneo la ufundi wakati wa mechi. Licha ya kuwa hakutaja jina la kocha yoyote lakini waandishi wa habari wakajua dhahiri anamlenga kocha wa Chelsea Antonio Conte na Jurgen Klopp wa Liverpool.

Jana ijumaa, Antonio Conte alipoulizwa kuhusu maneno hayo ya Mourinho alijibu kuwa Mreno huyo anaumwa ugonjwa wa kusahau alichokifanya nyuma (anapoteza kumbukumbu).
.
" Ninadhani inabidi ajione mwenyewe katika siku za nyuma , labda alikuwa anajisema mwenyewe katika siku za nyuma" alisema Conte .

Kocha huyo wa Chelsea akasema kuwa unaposahau tabia yako ya siku za nyuma unahitaji kuogopa kwa maana utakuwa unazeeka na hivyo unahitaji kufanyiwa uchunguzi wa kiafya.

Baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Deby Count katika FA Cup jana usiku, Jose Mourinho aliulizwa kuhusu alichosema Conte. Jose akaamua kuchukua vita hii kuipelekea Level nyingine .

" Kitu pekee ninataka kusema ili kumaliza stori hii ni kwamba ndio, nimefanya makosa katika eneo la ufundi siku za nyuma " amesema Mou.
.
"Ninafikiri nitaendelea kufanya machache. Ambacho hakijawahi kutokea kwangu , na hakitawahi kutokea  ni kufungiwa kwa kosa la kupanga matokeo . Hicho hakijawahi kutokea kwangu na hakitatokea kamwe ".

Jose Mourinho amesema hayo kwa kumbukumbu ya Antonio Conte kufungiwa miezi minne katika msimu wa 2012/13 akiwa Juventus kwa kosa la kuhusika katika upangaji wa matokeo ya mechi msimu wa 2010/11 wakati akiwa kocha wa Siena

0 comments:

Post a Comment