Wednesday, November 21, 2018

Kupitia ukurasa rasmi wa instagram ya Abdi Banda anayecheza soka la kulipwa nchini south afrika katika klabu ya Baroka fc amefunguka kuhusu taarifa zinazo enea mitandaoni kustaafu kuitumikia taifa stars.

" Napenda kuwaambia watanzania habari walizoziona au kuzisikia hazina ukweli. Bado umri unaniruhusu sana kulitetea taifa langu na kuitumikia timu yangu ya taifa kwa hiyo sijafikiria na sitokuja kufikiria kukaa pembeni kuitumikia timu ya taifa."

"Nadhani huu ni muda muafaka wa kulitetea taifa langu, nilisubiri kwa muda mrefu na sasa ndio wakati mwafaka wa mimi kuwa kwenye kikosi cha timu ya taifa au kujumuishwa katika timu ya taifa."

"Hayo maneno kuwa nimejiondoa au sitaki kuwa timu ya taifa ni habari za uzushi na ni watu ambao hawanitakii mema mimi na watanzania kwa ujumla." Ameandika hivyo banda.

0 comments:

Post a Comment