Kamati ya kuzuia na kupambana na dawa zisizoruhusiwa michezoni ya Kanda ya Tano Africa (RADO) imetoa hukumu ya kumfungia mchezaji Mohamed Issa kutokana na matumizi ya dawa zisizoruhusiwa michezoni aina ya Bangi
Disemba 9,2017 Mohamed Issa akiwa Machakos nchini Kenya alichukuliwa vipimo vya mkojo ambavyo vilisafirishwa kwenda kwenye Maabara ya WADA iliyopo Doha,Qatar kwa uchunguzi. .
.
Kwa mujibu wa Ibara ya 7.2 ADR inaelezea Mohamed Issa alivyokiuka ibara ya 2.1 ya RADO ADR ambayo inazungumzia kukataza matumizi ya dawa zisizoruhusiwa michezoni.
Alitakiwa kutoa maelezo ikiwemo kukataa au kukubali kosa ambapo Mohamed Issa alikubali mashtaka hayo kwa kukiri kosa akichagua kujitetea kwa njia ya maandishi,utetezi aliouwasilisha August 1,2018.
Baada ya uchunguzi wa maabara na utetezi wa Mohamed Issa,Kamati imemkuta na hatia na imemfungua kwa kipindi cha miezi 14 kuanzia Disemba 9,2018 na adhabu kumalizika Februari 8,2019.
Wakati wote akitumikia adhabu hiyo hataruhusiwa kufanya chochote kinachohusiana na mpira wa Miguu.Hatakiwi kufanya mazoezi hadharani,hatakiwi kuonekana akishiriki.
Alitakiwa kukutana na adhabu kubwa zaidi ikiwemo kufungiwa maisha lakini kamati kwa mamlaka iliyonayo imepunguza adhabu hiyo kufikia miezi 14 baada ya kumuona Mohamed Issa ni kijana mdogo.
Kamati ikijiridhisha kuwa anatumikia adhabu ipasavyo itamruhusu kuanza mazoezi na klabu yake katika miezi miwili ya mwisho katika adhabu yake.
Taarifa kwa Mujibu wa Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania Crifford mario Ndimbo.
0 comments:
Post a Comment