Manchester United na Chelsea wanatarajiwa kupigana vikumbo kuwania saini ya beki wa kushoto wa Barcelona Jordi Alba, kwa mujibu wa taarifa kutoka Marca.
Beki huyo wa kimataifa wa Hispania ana mkataba na Barcelona mpaka mwaka 2020 na kuanzia Ijumaa ya wiki iliyopita mpaka Jumatatu ya wiki hii kulitarajiwa kuanza kwa mazungumzo ya mkataba mpya lakini yamegonga mwamba.
Alba kwa sasa yupo kwenye kambi ya timu ya taifa kujiandaa kwa fainali za kombe la Duniani nchini Urusi.
0 comments:
Post a Comment