Tuesday, December 17, 2019

Uongozi wa Azam FC umethibitisha kumalizana na Yanga juu ya uhamisho wa mshambuliaji wake Ditram Nchimbi ambaye anakipiga kwa mkopo katika klabu ya Polisi Tanzania.

Afisa Habari wa Azam FC Jaffary Idd amesema Yanga walionesha nia ya kumuhitaji mchezaji huyo na na baada ya kufika mezani, walipewa masharti ikiwemo kulipa fidia ya muda wake wa mkataba uliobaki, sharti ambalo Yanga walilitimiza.

Inasemekana Yanga wametumia kiasi cha millioni 20 kuinasa saini ya Ditram Nchimbi na amesaini mkhataba wa miaka miwili.

0 comments:

Post a Comment