Kiungo wa Napoli Jorginho anaweza kuhamia Manchester City majira ya kiangazi kama vilabu hivyo vitaafikiana dili , kwa mujibu wa wakala wa kiungo huyo.
Taarifa kutoka Sky Sports zinasema kwamba Manchester City wameonyesha nia ya kutaka kumsajili kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26 na yupo kwenye orodha ya usajili ya klabu hiyo ya Etihad.
Napoli wanamthaminisha kiungo huyo kwa Pauni Milioni 53 ambaye bado ana miaka miwili katika mkataba wake.
Wakala wa Jorginho , Joao Santos amesema," Jorginho bado ana mkataba na Napoli lakini kama Napoli na Man City wataweza kukubaliana basi mchezaji atatua City."
. " Kuafikiana na klabu ya nchini Uingereza sio tatizo hasa ukizingatia umuhimu wa timu yenyewe."
" Lakini narudi hiyo itategemea na uamuzi wa Napoli kwasababu mchezaji bado ana mkataba pale wa miaka miwili zaidi."
0 comments:
Post a Comment