Friday, May 18, 2018

Awamu ya pili na mashindano yanayohusisha timu bora za Afrika Mashariki-SportPesa Super Cup yanatarajiwa kuanza Juni 3-10, 2018 nchini Kenya kwenye uwanja wa Kimataifa wa Moi uliopo Kasarani.

Timu zitakazoshiriki katika michuano hiyo kutoka Tanzania ni timu zinazodhaminiwa na SportPesa ambazo ni Simba, Yanga, Singida United pamoja na JKU (Jeshi la Kujenga Uchumi kutoka Zanzibar), wakati kutoka Nairobi timu zitakazoshiriki ni Gor Mahia, AFC Leopards na Kariobangi Sharks na Kakamega Homeboys.

“Matayarisho ya mwaka huu yamefanyika mapema na ukiangalia muda wa kupewa na taarifa mpaka kuanza ni zaidi ya mwa

“Kutakuwa na jumla ya timu nane za Afrika Mashariki na mshindi wa michuano hiyo atacheza na moja kati ya timu iliyoshiriki ligi kuu uingereza, Everton”

Timu zitakazoingia robo fainali kwenye mashindano haya watapata kiasi cha dola za kimarekani 2,500, nafasi ya nne timu itapata kiasi cha dola 5000, wakati nafasi ya tatu na wa pili dola 7,500 na 10,000 kila mmoja.

Timu itakayoshinda itazawadiwa kiasi cha dola 30,000 na kupata nafasi ya kuchuana na timu ya Everton katika uwanja wa Goodison Park


ka mmoja, hivyo basi hakuna sababu kwa timu zetu za Tanzania zisifanye vibaya zaidi ya mwaka jana kwani matayarisho yamefanyoka mapema na kwa hali hiyo timu zikifanya vibaya tutakuwa na sababu za kuwalaumu”

0 comments:

Post a Comment