Mchezaji wa Soka wa Liverpool na Raia wa Misri, Mohammed Salah ameumia bega na kuna uwezekano akakosa kucheza katika Michuano ya Kombe la Dunia 2018
Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la BBC, Salah ameteguka bega hivyo anaweza kukosa kushiriki Kombe la Dunia la mwaka huu
Inasemekana mtu aliyeteguka bega anachukua wiki 12 hadi 16 kupona kabisa. Kwa mfano, mchezaji Jamie Carragher aliyekuwa anachezea timu ya Liverpool alipata tatizo kama hilo katika msimu wa 2010/11 na alikaa nje kwa miezi miwili
Aidha, Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amenukuliwa akisema "Salah anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya X-ray na ni kweli anaweza kukosa kucheza Kombe la Dunia, ni majeraha yanayohusiana na bega".
0 comments:
Post a Comment