Sunday, May 27, 2018

May 31 2018, kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuondoka nchini kwenda Kenya kushiriki michunao ya SportPesa Super Cup.

Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema safari hiyo inasimamiwa na wadhamini wa michuano hiyo kampuni ya SportPesa.

Juzi wakati akihojiwa katika kipindi cha Yanga TV, Mkwasa alisema Yanga itaondoka Alhamisi, May 31 na kikosi cha wachezaji 20.

Mkwasa alisema msafara huo utajumuisha wachezaji wapya watakaosajiliwa na Yanga kwa ajili ya msimu ujao na kombe la Shirikisho barani Afrika.

0 comments:

Post a Comment