Sunday, May 27, 2018

Mjumbe wa Kamati wa Utendaji ya Yanga, Salum Mkemi imeelezwa kuwa bado ni kiongozi wa Yanga na hajajiuzulu kama ambavyo imekuwa ikienea katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

Baadhi ya taarifa katika mitandao hiyo ilikuwa kiripoti kuwa Mkemi amejiuzulu nafasi yake hiyo katika klabu ya Yanga ambayo kwa sasa inakabiliwa na changamoto mbalimbali za kiuchumi.

Mmoja wa viongozi wa Yanga ambaye ameomba kutotajiwa jina lake amesema kuwa Mkemi bado ni kiongozi wa klabu hiyo katika nafasi ya ya Ujumbe wa Kamati ya Utendaji. “Bado tupo na Mkemi na tunaendelea vizuri kabisa, huenda watu wamesikia wakaamini, maana  niliposikia nikazungumza naye na kasema hana huo mpango.” amesema kiongozi huyo.

Baadhi ya wanachama na mashabiki wamekuwa wakishinikiza ajiuzulu jambo ambalo yeye bado hajapatikana kulizungumzia.

0 comments:

Post a Comment