Saturday, July 28, 2018

Real Madrid wamesitisha mpango wa kumsajili Eden Hazard majira haya ya kiangazi ambapo kocha Julen Lopetegui anataka kumfanya Isco kuwa nguzo muhimu katika kikosi chake msimu mpya, kwa mujibu wa taarifa kutoka AS

Madrid wamekuwa wakihusishwa sana na Mbeligiji huyo tangu kuondoka kwa Cristiano Ronaldo .

Hata hivyo taarifa kutoka AS zinasema kwamba Madrid wamesitisha huo mpango kutokana na Lopetegui kumuamini sana Isco .

Madrid wanampenda sana Hazard lakini hawatomsajili huku wakitambua kwamba atagharimu kiasi cha Pauni Milioni 200 na wanaogopa kuziba njia ya kuboresha kipaji cha Marco Asensio , na kuamua kwamba hawatosajili ‘ Galactico ‘ majira haya ya kiangazi.

0 comments:

Post a Comment