Taarifa kutoka Sky Sports inasema kwamba Chelsea ni moja ya vilabu vitatu ambavyo vinawania saini ya mshambuliaji wa Manchester United Anthony Martial.
Taarifa zinasema kwamba Chelsea bado hawajawasilisha ofa rasmi lakini wana nia ya kutaka kumsajili Martial pamoja na vilabu vya Borussia Dortmund na Bayern Munich.
Martial kwa sasa yupo katika kikosi cha United kule Los Angeles kwenye maandalizi ya msimu mpya na amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake na amemuambia Jose Mourinho kwamba anataka kuondoka United.
Lakini taarifa kutoka Man United zinasema kwamba klabu hiyo haina mpango wa kumuuza Martial na Mourinho amesema kwamba atakuwa sehemu ya kikosi kitakachocheza mechi ya ufunguzi dhidi ya Leicester City.
0 comments:
Post a Comment