Beki wa kati wa klabu ya Baroka Fc Abdi Banda jana katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Afrika Kusini dhidi ya Wageni wao orlando pirates kwa mara ya pili alivaa kitambaa cha unahodha mara baada ya nahodha wao kupumzishwa katika mechi iliyomalizika kwa Baroka Fc kupigwa mabao 2-1
Ikumbukwe Banda kwa mara ya kwanza alivaa kitambaa cha unahodha katika dhidi ya Chippa United wakiwa ugenini na kupoteza kwa bao 1-0 katika mchezo uliopigwa Jumamosi Sept 15, 2018.
Mpaka sasa Banda anakuwa mchezaji wa kwanza kutoka Tanzania kupata unahodha katika Ligi Kuu nchini Afrika Kusini maarufu kama PSL.
0 comments:
Post a Comment