Wednesday, October 31, 2018

La Liga ipo mbioni kuandaa tuzo maalumu itakayokwenda kwa jina la gwiji wa soka wa Barcelona na duniani kwa ujumla Lionel Messi.

Tuzo kadhaa zimekwenda kwa majina kama makubwa kama Telmo Zarra, Rafael "Pichichi" Moreno na Ricardo Zamora.

Kutokana na mchango mkubwa alioonesha Messi ndani ya La Liga shirikisho hilo lina mpango wa kutoa tuzo moja ikiwa ni shukrani na heshima kwa uwezo wake.

Rais wa La Liga  Javier Tebas amesema la liga wataanza kutoa tuzo ya mchezaji wa thamani zaidi la liga [MVP] ambayo itajulikana kama 'The Lionel Messi Trophy'. Tebas "Nimewaza sana, nadhani Messi ndiye mchezaji bora katika historia ya La Liga, hana mpinzani na ni mfano wa kuigwa, hajawahi kushuka, kiwango chake ni kile kile" "Itakuwa jambo jema kutengeneza tuzo maalumu kila msimu ambayo tutaipa  jina la Messi"

Messi amekwisha kubeba la liga mara 9 na mwaka huu anatarajia kutafuta figa mbili yaani [10]. Messi, kufikia sasa amecheza mechi 427 na kufunga mabao 390 ndani ya La liga.

The Zarra Trophy [Mhispania mwenye magoli mengi]
The Pichichi Trophy [Mfungaji bora]
The Zamora Trophy [Goli kipa aliyefungwa magoli machache kulingana na mechi].

0 comments:

Post a Comment