Nemanja Matic atakosa mwanzo wa msimu wa Ligi kuu ya Soka ya Uingereza baada ya kufanyiwa upasuaji kwenye jeraha la tumbo ( abdominal injury ) .
Kiungo huyo alishindwa kucheza mechi ya ‘ Preseason ‘ ya kichapo cha 4-1 dhidi ya Liverpool.
“ Matic alirejea kutoka kwenye fainali za kombe la Dunia akiwa na jeraha na muda aliokuwa nao wa kupumzika baada ya kupewa likizo haukutosha kutibu tatizo.”
“ Alikwenda Philadelphia kuonana na mtaalamu na hakutoka katika Clinic na kwa haraka sana akafanyiwa upasuaji.”
Kiungo huyo wa kimataifa wa Serbia amerejea jijini Manchester kwa matibabu zaidi.
0 comments:
Post a Comment