Baada ya Hassani Kessy kutimkia Zambia, wengi tuliingia hofu kuwa safu ya ulinzi ya Yanga upande wa kulia itakuwa na wakati mgumu.
Juma Abdul anayetegemewa kwenye nafasi hiyo amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara, wengi tulikuwa na kila sababu ya kuwa na hofu.
Lakini baada ya kumuona kinda aliyepandishwa kutoka kikosi cha pili Paul Godfrey ambaye ndio kwanza ana miaka 17 akiitumikia Yanga kwenye michezo mitatu iliyopita, hakika kinda huyo anaweza kuwa mbadala wa Abdul.
Kiwango cha Paul kimekuwa kikiimarika kadiri anavyocheza kutokana na kuongeza kujiamini.
Paul aliyecheza mchezo dhidi ya Stand United na kufanya makosa mengi, ni tofauti kabisa na Paul aliyecheza mchezo wa jana dhidi ya Singida United.
Hiki ni kipaji kingine kimeibuliwa Yanga na kocha Mwinyi Zahera ameonyesha kumuamini na hahofii kumtumia kwenye kikosi chake.
0 comments:
Post a Comment