Wednesday, September 19, 2018

Cristiano Ronaldo ameoneshwa kadi nyekundu kwenye michuano ya klabu bingwa ulaya maarufu kama Champions League akiitumikia klabu yake mpya ya Juventus mara baada ya kukorofishana na mchezaji wa Valencia Jeison Murillo.
Mreno huyo amechukua taji hilo kwa miaka mitatu mfululizo akiwa na real madrid.  klabu yake mpya nayo ina njaa na kombe hilo lakini safari ya ronaldo msimu huu inaanza kwa ugumu.
Refa alipo muonesha kadi nyekundu ilimfanya atoe machozi uku akitoka nje taratibu. Hii ni kadi yake ya kwanza katika mashindano haya akiwa kama mfungaji bora wa mda wote.

Kutolewa kwake nje kutamfanya akosekane kati michezo kadha. Ronaldo atawakosa Young boys Bern pia atashindwa kurudi katika uwanja aliocheza zamani wa old trafford dhidi ya manchester united.

0 comments:

Post a Comment