Wednesday, September 26, 2018

Kocha wa Manchester United Jose Mourinho amesema kwamba hana tatizo na Paul Pogba licha ya kumuambia kwamba hatokuwa tena nahodha namba mbili.

. “ Ukweli pekee ni kwamba nimefanya uamuzi wa yeye kutokuwa nahodha namba mbili , lakini hatujagombana wala hakuna tatizo lolote.”

. “ Mimi ni Meneja ninaweza kufanya maamuzi kama haya , hakuna tatizo lolote wala hatujatofautiana , ni uamuzi ambao sihitaji kuelezea “.

Paul Pogba jana hakucheza mechi ya kombe la Carabao dhidi ya Derby alikuwa jukwaani ambayo United walipoteza. Wachezaji wengine ambao hawakuwepo kikosini kabisa  ni Luke Shaw, David De Gea, Antonio Valencia na Victor Lindelof ambao Mourinho amesema kwamba aliwapumzisha.

0 comments:

Post a Comment