Sunday, November 4, 2018

Wanachama wa Simba wakiongozwa na Kaimu Rais anayemaliza muda wake, Salim Muhene jana walipiga kura kuchagua Mwenyekiti na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa klabu ya hiyo, Boniface Lihamwike amemtangaza Swedi Khamis Mkwabi kuwa Mwenyekiti kwa kupata kura 1628 sawa na 97%

Walioshinda nafasi ya Ujumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ni Asha Baraka, Hussein Mlinga, Dkt. Zawadi Kadunda, Mwina Kaduguda na Seleman Said

Aidha, Crescentius Magori ametangazwa kuwa Afisa Mtendaji Mkuu(CEO) wa Kampuni ya Simba Sports Club

0 comments:

Post a Comment