Thursday, September 20, 2018

Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera amesema mchezaji wake Papy Tshishimbi anakosa nidhamu ya mchezo jambo linalopelekea kujichosha mwenyewe kutokana na kutekeleza majukumu ambayo si yake.

"Tshishimbi hana nidhamu ya mchezo anakimbia huku na huko, ulishawahi kumuona Ngolo Kante anapiga chenga? Kila mchezaji  anamajukumu yake uwanjani, Tshishimbi kazi yake akishanyang'anya mipira ni kutoa pasi lakini yeye anataka kuwa kama Messi akipata mpira anataka apige chenga."

"Matokeo yake anajichokesha mwenyewe kutokana na kukimbia sana lakini si kwamba perfomance yake imeshuka. Akitaka acheze vizuri bila kuchoka lazima awe na nidhamu ya mchezo."

0 comments:

Post a Comment