Rapa Kanye West na mke wake Kim K wametangaza rasmi kuhamia mjini Chicago nyumbani kwa Kanye West kama hatua ya kwanza ya safari yake kwenye SIASA.
Kanye West amethibitisha hili kwenye show na rapa Chance the Rapper 'Narudi Chicago na sitaondoka tena, alisema Kanye'.
TMZ wanasema Kanye na Kim Kardashian hawatauza mali zao mjini Los Angeles, wanahamia Chicago na watoto wao watatu North, 5, Saint, 2, and Chicago 'Miezi 8'.
Hatua ya kwanza ni Kanye kuhamisha ofisi zake za Yeezy kutoka Calabasas kuja Chicago, wachambuzi wa maswala ya burudani wanasema Kanye anahitaji kuanza maisha yake ya SIASA akiwa kwenye mji unaompenda wa Chicago.
0 comments:
Post a Comment