Tuesday, September 25, 2018

Manchester United wametangaza rekodi ya mapato ya mwaka ya zaidi ya Pauni Milioni 590 leo Jumanne ambapo Mtendaji Mkuu wa Man United Ed Woodward amesifia mafanikio hayo kuwa kielelezo cha United kusonga mbele zaidi.

Shukrani kubwa ya United katika mapato hayo ni kutokana  na ongezeko la mapato kutoka matangazo ya television ya miezi 12 kufikia Juni 30, 2018, pamoja na kumaliza nafasi ya pili katika ligi msimu uliopita tofauti na walivyomaliza nafasi ya sita misimu miwili iliyopita.


Katika kipindi cha miezi 12 iliyopita United walisaini jumla ya mikataba saba ya udhamini .

0 comments:

Post a Comment