Tuesday, September 18, 2018

Kocha msaidizi wa Simba Masoud Djuma kwa mara nyingine ameachwa Dar wakati kikosi cha Simba kikisafiri kwenda Kanda ya Ziwa kwa ajili ya michezo miwili dhidi ya Mbao (Mwanza) na Mwadui (Shinyanga).

Kocha mkuu Patrick Aussems amesema amemwacha Masoud ili awaandae wachezaji waliobaki Dar lakini pia amempa jukumu la kuwasoma Yanga watakapocheza kesho Jumatano dhidi ya Coastal Union kuelekea mechi yao ya September 30.

"Nimemuomba Masoud abaki Dar kusimamia mazoezi ya wachezaji waliobaki wakiwemo Juuko na Niyonzima kwa ajili ya kuwaandaa wawe fit kama wengine lakini pia kufatilia mchezo wa kesho Yanga dhidi ya Coastal Union."

Masoud pia hakusafiri na kikosi cha Simba kilichoenda Mtwara kucheza dhidi ya Ndanda FC.

0 comments:

Post a Comment