Juventus na AC Milan zinapania kumsajili kiungo wa kati wa Arsenal Aaron Ramsey. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 huenda akaondoka klabu hiyo msimu huu wa joto.
Arsenal iko tayari kumuuza Ramsey mwezi Januari isije ikaambulie patupu kwa kutoa bila malipo.(Mirror)
Barcelona inamfuatilia kiongo wa kati wa Manchester United na mfaransa Paul Pogba, 25, licha ya changamoto zinazomkabili katika klabu hiyo. (Independent)
Kuna hofu mvutano kati ya mkufunzi wa Man Utd Jose Mourinho huenda umewaathiri wachezaji wengine.
Antony Martial na Andreas Pereira wanadaiwa kushangazwa na mienendo ya hivi karibuni ya meneja wao Mourinho. (Mail)
Baadhi ya wachezaji wa United wamekasirishwa na hatua ya Mourinho kuwakosoa hadharani walinzi Eric Bailly na Phil Jones baada ya kushindwa na Derby katika kombe la Carabao Jumanne hii. (Sun)
Ajenti wa Pogba, Mino Raiola, anatarajiwa kukutana na maafisa wa United mwezi Novemba kujadili hatima ya siku zijazo ya kiungo huyo wa kati. (Guardian)
Mourinho amemkemea mshambuliaji wa Uingereza Marcus Rashford, mwenye umri wa miaka 20, kwa kushindwa kupumzika vya kutosha baada ya ushindi wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Young Boys wiki iliyopita. (Mail)
Kiongo wa kati wa Chelsea Cesc Fabregas ,anaamini itakuwa vigumu kwa klabu hiyo kuendelea kumkwamilia Eden Hazard.
Mchezaji huyo raia wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 27 alitaka kuondoka Stamford Bridge mwezi Julai lakini Chelsea ilisema haiko tayari kumuuza. (Evening Standard)
Kiungo mwenzake katika kilabu hiyo Ross Barkley amesema kwa sasa Hazard ni bora kuliko Lionel Messi wa Barcelona na Cristiano Ronaldo wa Juventus Cristiano Ronaldo. (Guardian)
AC Milan imeonyesha nia ya kumnunua Fabregas, 31, na imesema kuwa iko tayari kujishindia mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania mwezi Januari mwakani (Mundo Deportivo - kwa kihispania)
Kipa wa Everton kutoka Uingereza Jordan Pickford amesema tetesi zinazomhusisha na Chelsea msimu huu wa joto kamwe hazija athiri mipango yake.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ametia saini kandarasi mpya na klabu ya Toffees siku ya Jumatano. (Sky Sports)
Manchester City inamtaka kiungo wa kati Tanguy Ndombele anayechezea Lyon na timu ya France ya wachezaji wa chini ya miaka 21.
Mchezaji huyo ametia saini kandarasi ya miaka mitano na Ligue 1 mwezi huu. (Le10Sport -kwa kifaransa)
Real Madrid imeweka dau ya beki Benjamin Pavard lakini Stuttgart imekataa.
Manchester United na Arsenal pia waliwahi kuonyesha nia ya kumchukua mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 22. (Sport Bild kipitia Metro)
West Ham imeboresha ofa yake kwa Declan Rice, 19, baada ya kiungo huyo kukataa ofa yake ya awali ya kima cha zaidi ya euro 40,000 kwa wiki. (Telegraph)
Newcastle imekataa kuzungumzia uwezakano wa kumtafuta mtu atakayemrithi meneja wake Rafael Benitez, ambaye kandarasi yake inakamilika mwezi juni mwakani.
Hii ni kwa sababu klabu hiyo haijaonyesha ishara ya kumuachilia mhispania huyo kutoka uga wa St James Park. (Mirror)
Manchester United inajianda kumpatia euro milioni 60 beki wa kati Milan Skriniar, 23,kutoka Slovakia kuondoka Inter Milan. (Calciomercato - kwa kitaliano)
Meneja wa Fulham Slavisa Jokanovic amemwambia Harvey Elliott mwenye umri wa miaka 15 kujishughulisha zaidi na kazi ya ziada ya shule badala ya soka.
Kiungo huyo wa kati alikuwa mchezaji mdogo zaidi wa Fulham wakati walipoicharaza Millwall katika kombe la in the Carabao Cup siku ya Jumanne. (Times)
Kiungo wa kati wa Aston Villa, Jack Grealish anahisi kuwa angelipata nafasi katika kikosi cha England iwapo angelihamia klabu ya Tottenham msimu huu wa joto. Mchezaji huyo wa mika 23 hivi karibuni alitia saini kandarasi ya miaka mitano na Villa. (Telegraph)
'Huenda Sanchez akaondoka Man Utd'
Kiungo wa kati wa klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Uhispania Sergio Busquets, 30, nae ametia saini kandarasi mpya katika uga wa Nou Camp hadi mwaka 2023, hatua ambayo huenda ikaongeza thamani ya kumnunua hadi euro milioni 500 (AS)
Kip awa Paris St-Germain Gianluigi Buffon, 40, amsema mchezani mwenzake Marco Verratti,25, ndiye nyota halisi aliyesalia katka soka ya Italia. (Gazetta dello Sport - kwa kitaliano)
0 comments:
Post a Comment