Monday, October 8, 2018

Kupitia ukurasa wa instagram wa simba sc imethibitisha rasmi kuachana na kovha wao mnyarwanda msaudizi Masoud djuma 
"Kwa maslahi mapana ya klabu yetu, uongozi unawatangazia Wanachama na Washabiki wetu kwamba, kuanzia leo Jumatatu Tarehe 8/10/2018 tumesitisha mkataba na kocha msaidizi Irambona Masoud Juma baada ya kufanya mazungumzo baina ya pande zote mbili."

" Ni matarajio yetu mtaendelea kuunga mkono jitihada za uongozi katika kuboresha zaidi benchi la ufundi." simba sc

Kuna mvutano ulikuwepo kati ya koach mkuu na masoud djuma ulioanzia toka wapo kambini uturuki lakini tofauti hizo zilisuluhishwa na uongozi mapema tu kabla ya ligi kuanza.

Lakini baada ya mechi kadhaa tu tofauti ikaibuka tena. Ika mpelekea kocha mkuu kuomba achwe na wachezaji wa akiba na majeruhi timu ilipo safiri kwenda mikoani jambo lilo muumiza kwa kiasi.

Masoud Djuma alijua kabisa simba sc klabu itakuwa chini yake mara baada ya kuondoka kocha mfaransa iliyo pita. Lakini hali ikawa siyo shwari kwake akeletwa mbelgiji huy ambaye hawa elewani na hawa endani kiufundishaji.

Masud Djuma anaonekana hataki kufanya kazi nyuma ya mtu kwa kuwa anaajiamini ana uwezo wa kufundisha kama alivyo iongiza simba Mapinduzu cup na michuano ya Sport pesa kenya.

Kiujumla naona kuepukana na hili tatizo katika ligi. Vilabu visajili kocha mkuu ambaye amekamilika yaani awe tayari ana benchi lake la ufundi kuanzia kocha wa viungo, msaidizi na wa makipa ili waelewane katika utendaji wa kazi.

Na siyo kocha mkuu anasajiliwa huku na msaidizi kule wa makipa hapa hiyo italeta tofauti ya kimajukumu kazini.

Tumeshuhudia yanga nayo makocha wasaidizi kama Mwambusi akiondoka na Shadrack msajigwa hii yote ni kutofautiana kimajukumu na kocha mkuu.






0 comments:

Post a Comment