Wednesday, October 3, 2018

Nahodha wa klabu ya Manchester United Antonio Valencia  ameomba msamaha baada ya ku-like , post moja katika Instagram  ambayo ilikuwa na ujumbe wa kutaka Jose Mourinho kufukuzwa.

Post hiyo ambayo iliwekwa kupitia Ukurasa wa mashabiki wa Valencia ambao unaitwa 'teamvalencia25' baada ya mechi ya sare 0-0 dhidi ya Valencia ulisomeka," Hata sishangai na matokeo ya mechi ya leo ."

" Mara zote huwa natamani mechi zetu, lakini hivi karibuni Mourinho ametufanya kutuangalia sisi ni adhabu .. kuna kitu lazima kibadilike. Ni muda wa Mourinho kuondoka."

Ujumbe na picha yake , Antonio Valencia ali-like lakini sasa hivi ameomba msamaha  kupitia ukurasa wake wa Twitter kwa kusema:

"Jana nili-like , picha kwenye instagram bila hata kusoma ujumbe wake uliondena na picha husika. Huo sio mtazamo wangu na naomba msamaha kwa hilo . Namuunga mkono kocha wangu na wachezaji wenzangu. Wote tunajitoa kwa nguvu moja kuboresha matokeo."

0 comments:

Post a Comment