Wednesday, October 3, 2018

Yanga mambo ni moto hii ni baada ya kutoka suluhu na watani wao wa jadi Simba, sasa kocha Mkongo Mwinyi Zahera anakuja na mpango mkakati wa namna atakavyohakikisha anamaliza ngwe ya kwanza bila kufungwa.

Zahera amekiri kuwa mechi yao dhidi ya Simba, ilikuwa inamuumiza akili namna ambavyo mashabiki waliichukulia kwa uzito kiasi kwamba ilikuwa inampa picha ya kuona wametembea na matokeo mfukoni.

"Hii si kwa Yanga pekee, hata mashabiki wa Simba kwa namna walivyokuwa na shamla shamla na mechi hiyo inaona wazi kwamba wameishashinda kabla ya dakika 90. "Jambo ambalo ni changamoto kwa kocha wa aina yoyote Duniani kufanya ovyo mbele ya umati wa maelfu waliofika kuunga mkono timu yao, lakini pia endapo ukishinda mechi unaibuka shujaa, hilo lilinifanya nitumie mbinu za hali ya juu kuhakikisha hatupotezi mbele ya Simba."

Zahera anasema ligi itakapoanza baada ya timu ya taifa kumaliza majukumu yake, anaamini atakuwa na mbinu mpya ambazo zitamfanya mzunguko wa kwanza wajikite kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo .

"Nimejiwekea mikakati ya mzunguko wa kwanza nisipoteze. Nikifanikiwa nitaingia mzunguko wa pili kuelekea ubingwa, lengo ni kuona namna ambavyo tutafanya timu isipoteze mchezo hata mmoja ingawa tunajua kuna ushindani wa hali ya juu,"anasema Zahera.

Mwanaspot

0 comments:

Post a Comment