Tuesday, October 2, 2018

Mlinda lango wa Yanga Beno Kakolanya jumapili iliyopita aliibuka nyota wa mchezo wa pambano la watani wa jadi baada ya kufanikiwa kuzuia mashambulizi mengi langoni na kupelekea mchezo huo kumalizika kwa suluhu ya bila kufungana.

Kakolanya amesema siri kubwa ya mafanikio yake kwenye mchezo huo ni kuwa na utulivu langoni.

Amesema alijitahidi kufanya maamuzi sahihi kila alipotokea mipira lakini pia ushirikiano na wachezaji wenzake wa Yanga ulisaidia kwa kiasi kikubwa kufanya wapate matokeo hayo.

 "Nilibaini washambuliaji wa Simba walikuwa wana kasi hivyo nami nikawa nafanya uamuzi wa haraka kila nilipotokea mpira."

"Kwa kweli haikuwa rahisi lakini kwa ushirikiano na wachezaji wenzangu tulipata matokeo yake na kuweza kuondoka na alama moja ambayo sio mbaya kwetu."

Kakolanya pia amesema baada ya mchezo huo alipokea pongezi nyingi kutoka kwa wachezaji wenzake, viongozi, wanachama na mashabiki wa Yanga.

Kakolanya alituzwa zawadi mbalimbali zikiwemo fedha taslimu na WanaYanga kutokana na kazi kubwa aliyofanya kwenye mchezo huo.

Kiwango alichoonyesha juzi huenda kikampa nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha timu ya Taifa mbele na kipa wa Simba Aishi Manula ambaye kwa sasa ni chaguo la kwanza kwenye kikosi hicho.

Stars tayari imeingia kambini kujiandaa na michezo miwili ya kusaka tiketi ya kutinga fainali ya michuano ya AFCON 2019 dhidi ya Cape Verge

0 comments:

Post a Comment