Kikosi cha Yanga kinaendelea na mazoezi kwenye uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Mbao FC.
Mchezo huo utapigwa Jumapili ijayo, October 07 uwanja wa Taifa.
Baadhi ya wachezaji waliokosekana kwenye michezo ya iliyopita, Juma Abdul na Baruani Akilimali wamerejea kikosini baada ya kupona majeraha.
Juma Mahadhi aliyefanyiwa upasuaji wa goti hivi karibuni bado yuko nje.
Yanga pia inawakosa wachezaji wake watano walio kwenye kambi ya timu ya Taifa.
Hata hivyo wachezaji hao watarejea kikosini kwenye mchezo dhidi ya Mbao kisha kurudi tena Stars baada ya mchezo huo.
0 comments:
Post a Comment