Saturday, October 13, 2018


Klabu ya AS Monaco ya Nchini Ufaransa Imemtangaza Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Thierry Henry Kuwa Kocha Mpya wa timu hiyo.

Henry anakuja kuchukua Mikoba ya Kocha Leonardo Jardim ambaye amefukuzwa kazi Siku Chache zilizopita Kutokana na Matokeo Mabaya aliyoyapata Msimu huu.

Jardim ameingoza Monaco Kwenye Mechi 9 za Ligi na Mbili za Uefa Champions League, Katika Mechi 9 za Ligi Imeshinda Mechi 1 Imefungwa Mechi 5 Sare Mechi 2 Imefunga Magoli 9 Imefungwa Magoli 13 na Imepoteza Mechi zote  2 za Champions League.

Henry amesaini Mkataba wa Miaka Mitatu Kuifundisha timu hiyo.

0 comments:

Post a Comment