Saturday, October 6, 2018

Unaambiwa siku za Kocha Msaidizi wa Simba, Mrundi, Masoud Djuma zinahesabika kukaa ndani ya klabu hiyo baada ya kuelezwa kuwa bado hajawa na mahusiano mazuri na Kocha Mkuu, Mbelgiji Patrick Aussems.

Kwa mujibu wa gazeti la Spoti Xtra, limeeleza kuwa Aussems ameusisitizia uongozi kwamba hayuko tayari kufanya kazi na Djuma.

Habari zaidi zinasema kwamba Mbelgiji huyo alianza kutoelewana na Masoud tangu timu hiyo ikiwa kambini nchini Uturuki na waliporejea Dar es Salaam wakapatanishwa yakaisha lakini baadaye yakaibuka tena.

Via Spoti Xtra

0 comments:

Post a Comment