MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba, Elias Maguli amereja KMC na kusaini mkataba wa miezi sita kwa ajili ya kuichezea timu hiyo kwenye ligi kuu.
Awali Maguli alisaini mkataba na KMC katika dirisha kubwa mwaka huu lakini baadaye alipata dili la kwenda AS Kigali ya Rwanda ambapo aliwaomba KMC akajiunge na Wanyarwanda hao na akaruhusiwa.
Staa huyu kwa sasa ameamua kuvunja mkataba na AS Kigali na sasa amerejea tena kujiunga na watoto hao wa jiji, KMC.
0 comments:
Post a Comment