KMC ndiyo timu ya kwanza kufunga magoli mengi kuliko yeyote msimu huu 2020/21.
KMC 4-0 Mbeya City
Simba ndiyo timu ya kwanza kufungwa goli na timu iliyopanda daraja msimu huu.
Ihefu 1-2 Simba
Yanga ndiyo timu ya kwanza kutoka sare kwenye uwanja wa Mkapa msimu huu.
Yanga 1-1 Tanzania Prisons
Dodoma Jiji ndiyo timu ya kwanza kupata ushindi miongoni mwa timu zilizopanda daraja msimu huu.
Dodoma FC 1-0 Mwadui Fc
Azam ndiyo timu ya kwanza miongoni mwa wapigania ubingwa,kupata ushindi katika uwanja wa nyumbani.
Azam FC 1-0 Polisi Tanzania
JKT Tanzania ndiyo timu ya kwanza ya jeshi kupata ushindi msimu huu.
Kagera Sugar 0-1 JKT
Namungo FC ndiyo timu pekee itakayoiwakilisha nchi katika michuano ya kimataifa,iliyopata ushindi katika uwanja wa nyumbani.
Namungo 1-0 Coastal Union
Biashara UTD ndiyo timu ya kwanza kuifunga Gwambina msimu huu.
Biashara utd 1-0 Gwambina
NB: Jumla ya magoli 14 yamepatikana katika mzunguko huu wa kwanza,kati ya hayo 10 yamefungwa na timu zilizotumia viwanja vya nyumbani,magoli 4 yamefungwa na timu zilizotumia viwanja vya ugenini.
Bigirimana Braise wa Namungo fc amekuwa mchezaji wa kwanza kufumania nyavu msimu huu.
0 comments:
Post a Comment