Rasmi kiungo wa klabu ya Manchester City, Kevin De Bruyne ameanza mazoezi ya uwanjani baada ya kuwa nje kwa muda akiuguza majeraha yake ya mguu yaliomfanya kukosa mechi zote Saba za klabu yake msimu huu.
Kiungo huyo wa Kimataifa wa Ubelgiji aliumia mapema mazoezini kabla ya kuanza kwa mshikemshike wa Premier League msimu huu 2018-19, hali iliyopelekea kukosa mechi zote Saba ambazo klabu yake imecheza mpaka Sasa.
Kabla ya kupata majeraha hayo, KDB alitoka kuiwakilisha timu yake ya taifa ya Ubelgiji katika Fainali za kombe la Dunia nchini Urusi, ambapo walimaliza kwa kushika nafasi ya tatu nyuma ya Mabingwa Ufaransa na nafasi ya pili walikamata Croatia.
0 comments:
Post a Comment