Wednesday, October 3, 2018

Klabu ya Yanga imeandika barua kwenda Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wakieleza wanataka kuona TFF ichukue hatua kuhusiana na kitendo cha kiungo wa Simba, James Kotei.

Kotei alionekana akimpiga Gadiel Michael katika mechi ya watani Simba na Yanga, Jumapili iliyopita.

Msemaji wa Yanga, Dismas Ten amesema wameamua kufanya hivyo kama klabu wakionyesha wamekerwa wamekerwa na hali hiyo.

“Kama klabu hatuwezi kukaa kimya kwa vitendo ka hivyo vinatokea, tumeandika baraua"

“Sasa tutawaachia TFF wenyewe tuone kama wanachukua hatua au la, lakini sisi tumeonyesha namna tulivyokerwa na vitendo ambavyo si vya kiungwana,” alisema.

0 comments:

Post a Comment