Wednesday, November 21, 2018

Nahodha wa Yanga Kelvin Yondani na gokikipa Beno Kakolanya hawajasafiri na timu kuelekea Kanda ya Ziwa kwa ajili ya mechi dhidi ya Mwadui na Kagera Sugar. Inaelezwa sababu za wachezaji hao kutosafiri ni mgomo wakishinikiza kulipwa fedha wanazoidai klabu yao.

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Omary Kaya amesema hadi sasa bado hajapata taarifa rasmi juu ya tukio hilo.

"Mimi sijapata kauli ya Beno wala Kelvin, kwa hiyo kama ni majeruhi nitapata ripoti kutoka timu timu ya taifa ambayo itakwenda kwa daktari wetu."

"Kama itakuwa ni sababu nyingine pale nitakapokutana nao au kupata taarifa kutoka sehemu husika nitazungumza hilo lakini sidhani kama ni jambo la busara kumsemea mtu."

"Yanga timu nzima inadai, kama ni suala la kudai inawezekana inawezekana tatizo likawepo hata mimi naweza kusema nadai lakini kitu cha kwanza sio kugoma, ni kufanya kazi yangu na kufata taratibu muhimu za kupata stahiki yangu."

"Kwa hiyo watu wasipende kuzungumza kitu wasichokuwa na uhakika nacho lakini siwezi kumzuia mtu kusema kwa sababu kila mtu anazungumza chochote anauhuru huo ila kiofisi hakuna barua iliyokuja wala kauli ya Beno au Kelvin akisema siendi huko, nitakuwa naongopa."

"Kimsingi ni kweli hawajaenda na timu lakini siwezi kusema ni kwa sababu gani kwa sababu bado sijapata mawasiliano yao lakini ilikuwa waje waunganishe lakini inawezekana labda mtu ana udhduru wa kifamilia lakini ni hadi watakapopatikana na kusema ndio tutajua nini kitafuata baada ya hapo."

0 comments:

Post a Comment