Pep Guardiola amesema kwamba Kevin de Bruyne anafanyiwa uchunguzi na jopo la madaktari wa Manchester City baada ya kuumia goti lake la kushoto kwenye mechi ya Carabao jana usiku dhidi ya Fulham.
Guardiola amesema," Jeraha linaangaliwa na Madaktari . Kwa sasa sijui kama ni jeraha kubwa au kawaida tu."
De Bruyne alirejea dimbani siku kadhaa zilizopita baada ya kuumia goti lake la kulia ambalo lilimfanya akae nje ya dimba kwa muda wa miezi miwili.
0 comments:
Post a Comment