Friday, November 2, 2018

Mwamuzi wa Tanzania Jonesia Rukyaa amechaguliwa kuchezesha fainali za Afrika za Wanawake zitakazofanyika nchini Ghana.

Rukyaa amechaguliwa katika orodha ya waamuzi wa katikati akiwa ni mtanzania pekee.

Jumla ya waamuzi 13 wa katikati wamechaguliwa na waamuzi wasaidizi 12.

Fainali hizo pia zitatumika kupata timu zitakazoiwakilisha Afrika kwenye fainali za kombe la dunia kwa wanawake zitakazofanyika mwakani Ufaransa.

Washindi watatu wa juu ndio watafuzu kucheza kombe la dunia.

0 comments:

Post a Comment