Wednesday, November 21, 2018

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera sio mtu wa kukaa kimya pale anapoona mambo hayaendi sawa.

Pengine utaratibu huu wa Zahera huenda ukaisaidia Yanga kwa viongozi wake kuweka wazi changamoto zinazokuwa zinaikabili timu hiyo kabla ya mambo kuharibika zaidi

Zahera tayari ametua nchini na yuko Shinyanga na kikosi cha Yanga kinachojiandaa kuikabili Mwadui Fc kwenye mchezo wa kiporo wa ligi kuu ya Tanzania bara hapo kesho.

Mcongomani huyo amesema ukiondoa wachezaji majeruhi, kikosi chake kinawakosa nahodha Kelvin Yondani na mlinda lango namba moja Beno Kakolanya 'waliogomea' safari kutokana na kuwa na sababu binafsi.

Zahera amesema wachezaji hao wanadai malimbikizo ya mishahara ya miezi MITANO na wamekataa kusafiri wakishinikiza walipwe fedha zao.

Miezi mitano ni mingi nadhani haitakuwa jambo jema kuwalaumu wachezaji hao kwani watakuwa wamevumilia sana!

Kuhusu suala la usajili wa wachezaji wapya Zahera amesema ni bora Yanga ikajikita katika kuboresha maslahi ya wachezaji waliopo kuliko kusajili wachezaji wapya halafu timu ikaishia 'kuwakopa'

Kulingana na mtandao wa Mwanaspoti, Zahera amewaandikia ujumbe kuelezea changamoto zinazoikabili Yanga sasa.

Kocha Zahera ameandika ujumbe wake kwa Kiswahili cha tabu kilichochanganyika na kikongo kuhusu sakata hilo:

Salama vituyote ni vizuri kuanguvu ya munyezi mungu.Team ili fika vizuri apa shinyanga.na mimi nalikuta team apa shinanga

Ila wamenipasha kama watchezaji wawili wamekataha kusafiri sababu ya mwezi tano ya mishahara yaho awapewe .kevin yondani .na BENO gool keeper

Nazani nyinyi wote munangoja kuniuliza abari kocha dirisha kidogo imefunguliwa ni je? Ku ngambo ya yanga? Ile nyinyi wite munangoja niwape abari.

Aya mimi nasema kua kupata mchezaji mupia inaomba transfert.inaomba kusikilizana mshahara.kusikilizana modaliti ya contrat na ile yote kuasikuyaleo sione hata namna moja yakuweza kusumulia na wachezaji wowote sababu atueneze ile ma conditions na waeleza.

Uta anzia wapi ? Na utamalizia wapi masungumzo na watchezaji wa mpia ? Viongozi wengine wameniambia nitafute watchezaji.sasa limi nitafute muchezaji nisumulie naye nini?

Wakati team aieneze ma conditions.ya transfert .ya vitu yote inaomba kua kununua m

0 comments:

Post a Comment