Friday, November 23, 2018

Mchezaji wa zamani wa Arsenal Nicklas Bendtner anatarajia kwenda kutumikia kifungo jela kwa muda wa siku 50 kwa kosa la kumshambulia dereva Taxi.

Mdenmark huyo,30, anayecheza ligi ya Norway katika klabu ya Rosenborg anaenda jela baada ya kuifuta rufaa yake aliyoikata baada ya hukumu kutoka mapema mwezi huu.
Hata hivyo haijawekwa wazi ni lini atakwenda kutumikia kifungo hicho.

Bendtner alivunja taya ya dereva huyo mwezi Septemba huko Copenhagen na mahakama ikaoneshwa video ya tukio hilo kutoka ndani ya taxi.

Bendtner alikataa kumlipa dereva nauli ya Pauni 4.8 ( Tsh 14,000) na baadae kuanza kumpiga,kabla ya kuendelea kumpiga akiwa amedondoka chini.

Bendtner alikiri kumpiga dereva huyo, ingawa alidai alikuwa anajilinda “ Nilikabiliana nae kwa kujilinda “ Mchezaji huyo alisema mahakamani. “ Nilidhani dereva angeweza kuniumiza. Kwani tulikuwa tunagombana. Tuliinua mikono yetu kwa pamoja, na mimi ndiye niliyewahi kumpiga “
Mahakama pia ilimtaka Bendtner kumlipa dereva huyo pauni 1000 ( Milioni 2.9) kama fidia.

Mdenmark huyo aliomba msamaha mbele ya waandishi wa habari siku tatu baada ya tukio.

Bendtner akiomba msamaha alisema : “ Nilihusika katika tukio hili la bahati mbaya. Sikufahamu litafikia kama hivi, na ni kweli nina huzuni kubwa kwamba matokeo yake  yamekuwa ya bahati mbaya kama nilivyofanya. “

0 comments:

Post a Comment