Wednesday, January 2, 2019

Jina la mlinda lango Ibrahim Ahmed aliyetua Yanga wakati wa dirisha dogo la usajili akiwa mchezaji huru, limejumuishwa katika kikosi cha Yanga kilichokwenda Zanzibar kushiriki michuano ya kombe la Mapinduzi.

Ibrahim atakuwa na nafasi ya kuonyesha uwezo wake kwenye michuano hiyo na pengine kumshawishi kocha Mwinyi Zahera ili amtumie katika michezo ya ligi kuu ya Tanzania Bara na kombe la FA.

Kwa sasa Yanga inawategemea walinda lango wawili tu Ramadhani Kabwili na Klaus Kindoki baada ya kocha Zahera kumuengua Beno Kakolanya

Usajili wa Ibrahim kutua Yanga uligubikwa na sintofahamu nyingi baada ya Zahera kubainisha kuwa mlinda lango huyo aliyekuwa akicheza soka la ufukweni alisajiliwa bila ya yeye kufahamu.

Hata hivyo huenda michuano hii ya kombe la Mapinduzi ikamaliza utata hasa kama ataonyesha uwezo mkubwa.

0 comments:

Post a Comment