KISWAHILI KILIMLETA ZAHERA YANGA
Nilifuatwa na watu wa timu ya Buildcom ya Zambia. Nikaenda kufanya nao mazungumzo, nikakubaliana nao.
Lakini kabla ya kusaini mkataba, mdogo wangu akanipigia simu kwamba kuna timu kubwa ya Tanzania inanitaka.
Nikashangaa, kuna timu kubwa kutoka Tanzania? Nilikuwa sijawahi kusikia kwamba Tanzania kuna timu kubwa. Timu kubwa za Afrika nilizokuwa nazijua ni TP Mazembe, Al Ahly na Esperance.
Akaniambia hiyo ni timu kubwa sana. Nikamwambia mimi nina misimamo yangu, nikishaamua kitu, nafanya hicho hicho na nilishaamua kufanya kazi na Buildcom.
Akasema, "kaka, njoo Tanzania. Huko Zambia utapata tabu sana kwa sababu wanaongea kiingereza na wewe hukijui. Tanzania wanaongea Kiswahili ambacho unakijua...njoo huku.
Hapo ndipo akili zangu zikagonga...nikaona kweli, huku Zambia nitapata tabu. Nikaachana na Buildcom na kuja Tanzania kuifundisha Yanga. -Mwinyi Zahera, kocha mkuu wa Yanga SC.
0 comments:
Post a Comment