Hakuna ubishi Azam fc walistahili kutwaa hiki kombe kwa namna yeyote ile, Waliwekeza nguvu kubwa sana.
Hawakuwa na cha kupoteza Mapinduzi cup, ndiyo maana hawa Walichezesha full mkoko , hakuna ingizo jipya toka kikosi "B".
Napata wasisi sana juu ya utimamu wa mwili kwa wachezaji wa Azam kwa michezo ijayo ya ligi kuu. Mapinduzi cup ilikuwa ni bandika bandua hakuna mda wa kutosha wa kupumzika.
Ukizingatia wachezaji ni wale wale wanao pata na nafasi ligi kuu na tegemezi ndio hao hao walio cheza michezo yote mapinduzi cup.
Naona mazingira Miundo mbinu itawachosha zaidi kwa michezo ijayo, watahitajika kutoka nje ya dar tena azam fc wao hutumia bus lao nadra sana kupanda ndege.
Kila mmoja anajua mzunguko wapili ulivyo mgumu , Azam inampasa akapambane sana lakini kwa usalama wa wachezaji lazima wa changanye na kikosi kile ambacho hakikupata nafasi mapinduzi cup.
0 comments:
Post a Comment