Mshambuliaji wa Azam fc na Taifa Stars, Yahya zaid ameomdoka jana Dar es Salaam kwenda Misiri kujiunga na klabu ya Ismailia ya Misri.
Inaelezwa Zayd atasaini mkataba wa miaka mitatu kuitumikia Ismailia baada ya kumalizana na Azam FC juu ya mchezaji huyo ambaye alikuwa amebakiza mkataba wa miaka miwili Azam Complex.
Endapo atajiunga na Ismailia ataungana na nahodha wake wa zamani wa Azam Himid Mao katika ligi ya Misri, Himid anaichezea Petrojet.
0 comments:
Post a Comment