Majonzi yameikumba tena familia ya mchezaji Emiliano Sala aliyefariki miezi mitatu iliyopita baada ya baba mzazi wa mchezaji huyo Horacio Sala kufariki dunia leo akiwa na umri wa miaka 58 katika mji wa Progreso nchini Argentina.
Baba huyo mzazi wa Emiliano amekuwa kwenye matibabu ya moyo kwa kuwa hakuwahi kuamini kama mwanaye amefariki japo alikuwa ni sehemu ya maziko ya kijana wake aliyefariki akiwa na miaka 28.
Emiliano Sala aliyekuwa akiitumikia Nantes FC alifariki kwa ajali ya ndege alipokuwa akitoka Ufaransa kwenda England kujiunga na timu yake mpya Cardif City.
0 comments:
Post a Comment