Ronaldo ameweka rekodi ya kuwa mpiga Faulo ( Free - kick ) Mbovu namba mbili kuwahi kutokea katika ligi kuu italia maarufu kama Serie A.
Ronaldo amepiga mikwaju 18 kwa michezo ya Seria A Tangu ajiunge na juventus. Lakini ukijumlisha na zile Free- kick sita za Champions league zinakuwa 24.
Katika hizo free-kick 24 , 15 zilibamiza ukuta , 7 ziliokolewa na walinda milango na 2 alikosa shabaha kabisa ( alipiga minazi ).
Anaye shikilia nafasi ya kwanza kwa upigaji mbovu wa free-kick ni anaitwa Camillo ciano alipiga free-kick 21 mfululizo pasipo kufunga goli kwa kipindi chote alichocheza italia akiwa na Napoli.
NB: Cristiano ronaldo akiwa Real madrid aliPiga free-kick 313 na kufanikiwa kufunga 20 tu. ⚫️
[ source The sun ]
0 comments:
Post a Comment