KOCHA wa Timu ya Taifa Brazil Tite,amesema kwamba hawezi kushindwa katika michezo yake mara baada ya kumpoteza nyota wake Neymar ambaye ni majeruhi.
Neymar, mwenye miaka 26,alifanyiwa upasuaji wa mguu baada ya kuumia katika mchezo wa ligi kati ya Paris Saint-Germain dhidi ya Marseille mwezi Februari.
Wakati ambapo Neymar anatarajia Kuwa mmoja wa wachezaji ambao wataiongoza Brazil katika Fainali za Kombe la Dunia, Brazil inakabiliwa na Urusi siku ya leo na siku nne baadae watacheza na Ujerumani katika michezo ya kirafiki kwaajili ya maandalizi bila Neymar.
Tite alisema hakuna njia, tayari Neymar hayupo kikosini hakuna sababu ya sisi kushindwa "Douglas Costa atapambana katika nafasi hiyo na atacheza yeye kama yeye". "Pamoja na hilo nitamtaka Casemiro, afanye jukumu lile ambalo anafanya akiwa na Real Madrid," alisema Tite.
0 comments:
Post a Comment